Yanga kuanza mazoezi kesho bila wachezaji hawa

0
5
Kikosi cha Yanga kinarejea mazoezi kesho kujiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Singida United.
Wachezaji wa timu hiyo walipewa mapumziko ya muda mfupi ikiwa siku kadhaa baada ya kurejea kutoka Botswana kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.
Yanga itaanza tena mazoezi kesho zikiwa zimesalia siku 6 pekee kabla ya kucheza dhidi ya Singida United Jumapili ya Aprili Mosi kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida.
Kuelekea mazoezi hayo, wachezaji Ramadhan Kabwili, Kelvin Yondani, Hassan Kessy, Ibrahim Ajib na Gadiel Michael watakosekana.
Wachezaji hao wapo kwenye kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars, inayojiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Jumanne ya wiki hii.
Source:Saleh Jembe.
         
Imeletwa na agape patrick
  Email agape@spoti.co.tz

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here