Wawakilishi wa Tanzania Madola hawataki masihara

0
3
NYOTA wote watakaoiwakilisha nchi kwenye Michezo ya Madola tayari wako Dar es Salaam na wanachosubiri ni hafla ya kuagwa tu kesho Jumanne tayari kwa safari ya Australia itakayoanza Alhamisi.
Mwanariadha, Anthony Mwanga aliyekuwa Afrika Kusini, Ally Gulam aliyekuwa  Brunei, muogeleaji, Sonia Tumiotto aliyekuwa Uingereza na Hilal Hilal aliyekuwa Dubai wote wako Dar es Salaam sanjari na wanariadha waliokuwa kambini Arusha wanachosubiri ni safari tu.
Kocha Zacharia Barie amesema hana presha na kikosi chake na kuwatoa hofu Watanzania kuwa nafasi ya medali ipo.
Kocha wa kuogelea, Khalid Lushaka amesema anaamini vijana wake watafanya vizuri kutokana na maandalizi waliyokuwa wakifanya kwenye klabu zao nje ya nchi.

Chanzo:mwanaspoti

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here