Ukinifungia nyimbo hainipunguzii kitu, tusifanye kwa kukomoana – Diamond

0
4

Msanii wa muziki Bongo, Diamond amefunguka kuhusu kufungiwa kwa nyimbo zake mbili ‘Waka na Hallelujah’ kwa kueleza kuwa ni kitu ambacho hakiwezi kumpunguzia chochote na hakiwezi kujenga muziki wa Tanzania.

Muimbaji huyo ameiambia The Playlist ya Times Fm kuwa yupo tayari kupigania muziki wake kwa lolote lile na iwapo kuna sehemu ambayo wao kama wasanii wanaenda kinyume ni jambo la kuelekezana.

“Suala si kufungia tu nyimbo, mimi ukinifungia nyimbo hainipunguzii kitu nikienda nje naenda nai-perform ukiwa hutaki sinaondoka tu naenda nchi nyingine, kwa hiyo ni kukaa tuzungumze, tuelekezane lakini tusifanye kama kukomoana, hapana, tufanye katika mazingira ambayo yatasaidia sanaa ikue,” amesema.
“Bongo Flava naijua kweli kweli, halafu kama mimi ni mtu ambaye siogopi kwenda jela kwa ajili ya Bongo Flava, siogopi kufanya chochote kwa sababu ndio Baba yangu na Mama yangu ndio nimefanya hadi nimefika hapa, kwa hiyo unapo-deal na sanaa yangu hakikisha unafanya kitu ambacho kipo sahihi usikurupuke kwa sababu una mamlaka,” amesisitiza.
Katika hatua nyingine Diamond ametaja kiasi cha fedha alichotumia katika kuandaa stage ambayo ilitumika katika uzinduzi wa albamu yake ya mpya ‘A Boy From Tandale’ uliyofanyika Nairobi nchini Kenya, Diamond amesema stage hiyo iligharimu zaidi ya Tsh. Milioni 150.


Na Mwanahabari wetu: Richard Shiyo Barua pepe richard@spoti.co.tz

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here