Transfer Updates: Spurs yakubali yaishe kwa beki wao kisiki raia wa belgium.

0
6
Tottenham hotspurs watalazimika kumuuza beki wao Toby Alderweireld ambaye mkataba wake unaisha mwishoni  mwa msimu ujao. spurs na mchezaji huyo wameshindwa kukubaliana katika kusaini mkataba mpya na sasa ili kupata faida Spurs watalazimika kumuuza beki huyo wa Belgium ambaye anacheza timu moja na Eden Hazrd wa Chelsea katika timu ya taifa Spurs wamekubali kumuuza beki huyo
kwa ada ya angalau Paundi 44 million. na kama ataendelea kubaki kuichezea spurs mpaka kufikia January 1 2019, kuna kipengele kwenye mkataba wake ambacho kinamruhusu kuondoka Spurs kwa kiasi cha Paundi 25 ml ambacho kitalipwa na timu yoyote itakayo mhitaji Toby.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here