TFF Yafunguka Kuhusu Kocha Mpya Wa Taifa Stars

0
3

Wakati Watanzania wengi wakijiuliza juu ya mwelekeo wa timu yao ya taifa katika mchezo wa soka, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeanika wazi vigezo vipya watakavyovizingatiwa katika mchakato wa kutafuta kocha mpya wa timu hiyo.
TFF imeweka wazi kuwa tayari imeshaanza kupitia ‘CV’ mbalimbali walizopokea zitakazowafanya kumpata kocha mpya atakayechukua mikoba ya kocha wa sasa wa timu hiyo, Salum Mayanga.
Shirikisho hilo limeamua kuchukua maamuzi hayo ya kutafuta kocha mpya baada ya mkataba wa kocha wao wa sasa Mayanga kumalizika tangu mwezi uliopita, lakini amekuwa akiendelea kukitumikia kikosi hicho kwa maombi maalumu.
Alipoulizwa juu ya suala hilo, Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidau aliweka wazi kuwa ni kweli Mayanga ameendelea kuitumikia Taifa Stars kwenye michezo miwili ya kirafiki iliyopo kwenye kalenda ya Fifa licha ya mkataba wake kuwa umeshamalizika.
Amesema kuwa TFF tayari ipo katika mchakato wa kuhakikisha inampata kocha mpya ambaye atakuwa na vigezo vya kuifikisha Taifa Stars katika levu ya juu zaidi ya ilivyo sasa.
Kidau amesisitiza kuwa uongozi wa TFF umejipanga kikamilifu kuhakikisha soka la Tanzania linafika mbali na ndiyo maana karibia michuano yote ya kimataifa vikosi vya taifa vinashiriki na TFF inafanya kila liwezekanalo ili kufuzu kwa kila hatua inayoendelea mara tu baada ya kuingia katika michuano mbalimbali.
Kidau amesema kwa kuwa walimu wapo wengi wenye viwango, itategemea na hao wanaopitia majina maana makocha ni wengi pia waliotuma CV zao.

by richard@spoti.co.tz

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here