Tambwe Yuko Fiti, Anarudi Kupigania Ubingwa Yanga

0
5

Yanga inalingana pointi na Simba katika msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom lakini Simba ipo juu kileleni kutokana na wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Sasa wakati vita hiyo ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom ikiendelea kukolea, Yanga wameanza kupata nafuu baada ya wachezaji wao kadhaa kurejea kwenye kikosi cha kwanza baada ya kuwa majeruhi kwa muda mrefu.
 Straika wa timu hiyo, Amissi Tambwe ambaye amekuwa majeruhi kwa muda mrefu, amesema ameanza kurejea katika afya nzuri na tayari ameanza mazoezi ya gym.
Tambwe ni miongoni mwa majeruhi wa Yanga ambao wameifanya timu hiyo kupitia kipindi kigumu kutokana na nyota wake wengi kuwa nje akiwemo Donald Ngoma na Thabani Kamusoko ambao wamerejea uwanjani.
Tambwe ambaye ni mchezaji wa zamani wa Simba, amesema kwa sasa anaendelea vizuri na ana matumaini ya kurejea uwanjani hivi karibuni.
Amesema kuwa muda si mrefu atarejea uwanjani kwani maendeleo yake ni mazuri tofauti na ilivyokuwa wiki kadhaa zilizopita.
Ikiwa Tambwe atarejea katika ubora wake baada ya kusumbuliwa na goti kwa muda mrefu, akiungana na kina Kamusoko na Ngoma, ni jambo zuri kwa Yanga katika mbio hizi za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacoma na katika michuano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho pamoja na Kombe la FA ambapo kote inashiriki.

by richard@spoti.co.tz

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here