Tambwe arejea kamili Yanga

0
9
MSHAMBULIAJI wa Yanga Amissi Tambwe ameanza mazoezi taratibu lakini akasema kama kuna kitu amekimisi ni kufunga mabao hasa akiangalia mechi za timu yake.
Akizungumza na Mwanaspoti Tambwe alisema wiki hii ameanza mazoezi ya gym baada ya kidonda cha pasuaji wake kupona vyema na daktari kumruhusu kuanza mazoezi.
Tambwe alisema ingawa ameanza mazoezi lakini bado hataweza kuwahi mechi mbili za timu yake za sasa Kimataifa dhidi ya Welayta Dicha ya Ethiopia watakayokutana nayo katika mchezo wa kwanza nyumbani Aprili 7.
Alisema kama kuna kitu kinamuumiza sasa ni kukosa mechi hizo ambazo anaamini kama angekuwa sawa angetoa mchangop mkubwa kwa kuwa timu wanazokutana nazo zinafungika.
 NA Vicent Segona vicent@spoti.co.tz
Chanzo: Mwanaspoti

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here