Simba yatua kwa kishindo Port Said kuivaa Al Masry

0
5
Cairo, Misri. Mabingwa mara 18 wa Ligi Kuu Bara, Simba wamewasili salama jijini Cairo, Misri na kuondoka mara moja kuiwahi Al Masry mjini Port Said.
Simba iliwasili Cairo saa 8 usiku kwa muda wa hapa (saa 9 usiku kwa Tanzania) na kukamilisha taratibu za kuondoka Uwanja wa Ndege wa Cairo saa 9.30 usiku.
Hata hivyo, mabosi wa Simba wakiongozwa na Kaimu Rais, Salim Tryagain walihakikisha msafara unaondoka Cairo muda huo huo, ili kuwahi Port Said yalipo Makao Makuu ya Al Masry umbali wa Km213.
Katika mazoezi yao ya mwisho Dar es Salaam, kocha Pierre Lechantre, alionekana kusisitiza wachezaji wake wapige pasi za haraka ili waweze kupata bao.
Lechatre alikuwa hataki kabisa kuweka mpira nyuma, mara kwa mara alikuwa akiwakomalia mabeki wake Erasti Nyoni na Yusuf Mlipili wasikae na mipira nyuma, badala yake wawaishe mbele.
Source: Mwanaspoti

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here