Simba nao kuanza mazoezi bila wachezaji wao hawa muhimu wa kimataifa

0
8


Na George MgangaWekundu wa Msimbazi, Simba SC, jana wameanza mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Njombe Mji FC, utakaopigwa kwenye Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe, Aprili 3 2018.
Mazoezi hayo rasmi yameanza kufuatia kikosi hicho kupewa mapumziko ya siku kadhaa baada ya kuwasili nchini kutokea Misri kwa ajili ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Kikosi hicho kimeanza mazoezi hayo jana bila uwepo wa mshambuliaji wake Emmanuel Okwi pamoja na beki Juuko Murushid waliosafiri kwenda Uganda kuitumikia timu yao ya taifa ‘The Cranes’.Okwi na Murushid waliisaidia timu yao kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 katika mchezo wa kirafiki wa kalenda ya FIFA uliopigwa jana dhidi ya Sao Tome ambapo Murushid alifunga goli moja.
Kuelekea mchezo huo wa kiporo dhidi ya Njombe, Simba ipo kileleni mwa msimamo ikiwa na alama 46 sawa na Yanga, ingawa Simba ina faida ya mabao ya kufunga na kufungwa.Source: Saleh Jembe
Email: agape@spoti.co.tz

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here