Serengeti yaikandamiza Twiga Stars

0
9

TIMU ya soka ya Taifa ya Wanawake, Twiga Stars jana ilipokea kipigo cha mabao 4-1 kutoka kwa timu ya Taifa ya Vijana walio chini ya miaka 17, Serengeti Boys katika mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.

Katika mchezo huo, Serengeti Boys walionekana kuwatesa dada zao kwa kupigiana pasi moja moja na kuwalazimisha kucheza nusu uwanja na pale walipotaka kufanya shambulizi la kushtukiza, walizidiwa mbio.

Bao pekee la Twiga lilifungwa na mshambuliaji mwenye mbio mithili ya duma, Mwanahamisi Omari kwa penalti baada ya kufanyiwa madhambi kwenye eneo la hatari.

Akizungumza baada ya mchezo huo kocha msaidizi wa Twiga, Edna Lema alisema anashukuru kwani unampa nafasi ya kujua mapungufu ya kikosi chake kabla ya kuikabili She Polopolo ya Zambia Aprili 4 kwenye mchezo wa kufuzu kwa mashindano ya Mataifa ya Afrika, Afcon.

“Tunaendelea vizuri na mazoezi, nashukuru kupata mchezo huu kwani tulitaka kuiangalia timu inavyocheza, Serengeti haijatuzidi sana tofauti wao ni wavulana,” alisema Edna Serengeti Boys inajiandaa na mashindano ya CECAFA ambayo yanatarajiwa kuanza Aprili 1-15 nchini Burundi.

Chanzo:Habrileo

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here