Samatta amtia moyo Msuva

0
8

MSHAMBULIAJI wa Genk na Taifa Stars, Mbwana Samatta amemwambia Simon Msuva asiwe na shaka kupangiwa na TP Mazembe kwenye kundi moja michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika, kwani timu yake itatoboa tu.

Msuva amejikuta kwa mara ya kwanza akiangukia kwenye hatua ya makundi ya michuano hiyo, baada ya timu yake Difaa Hassan El Jadida kupangwa kwenye Kundi B ikiwa pamoja na TP Mazembe, Mouloudia Club D’alger na ES Setifienne.

Kutokana na uzoefu wa mkali huyo anayekipiga ligi ya Ubelgiji alisema kundi hilo ni gumu sana, lakini kwa kuwa tayari Msuva amecheza michezo kadhaa na kuwafahamu vizuri waarabu haitampa shida.

“Nimeangalia makundi yote lakini inaonekana kundi lao ndio lenye uzito, lakini kwa sasa Msuva ana uzoefu wa pande zote mbili kwa sababu anacheza katika nchi ya kiarabu kwa hiyo amezoea hali ya soka la kiarabu,” alisema Samatta.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba alisema TP Mazembe haitakuwa na utofauti mkubwa sana na As Vita ya Kongo ambayo waliiondoa kwenye hatua ya awali kwa sababu mpira wa nchi moja una tabia ya kufanana.

Alisema hakutakuwa na utofauti kubwa tamaduni zao zitakuwa zinafanana kwa kiasi fulani, muda watakaokuwa wanacheza nadhani utakuwa ni sawa na ule ambao wanacheza wakiwa Morocco kwa hiyo hali ya hewa haitokuwa tofauti sana.

Chanzo:Habarileo

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here