Rwanda watamba kutetea taji la Taekwondo

0
9

KOCHA Mkuu wa timu ya taifa ya Rwanda ya Para Taekwondo, Irene Bagire ana matumaini ya timu yake kufanya vizuri hadi kutwaa ubingwa wa Afrika katika mashindano yatakayofanyika Machi 30 hadi Aprili 1 katika jiji la Aigdir, Morocco.

Timu za taifa za Para Taekwondo na Taekwondo zilizoondoka nchini mwishoni mwa wiki na kwenda Morocco kwa ajili ya mashindano hayo ya Afrika ya Taekwondo.

Mashindano hayo yatafanyika kuanzia Machi 28-30 wakati yale ya Para Taekwondo, ambayo ni maalumu kwa ajili ya watu wenye ulemavu, itaanza siku moja baadaye.

Rwanda ambao walikuwa wenyeji wa mashindano ya Para Taekwondo mwaka jana, walimaliza kileleni katika msimamo wakiwa na medali sita, zikiwemo mbili za dhahabu tatu za fedha na moja ya shaba.

“Baada ya miezi mitatu ya mazoezi ya nguvu, sasa tuko tayari kwa ajili ya kusaka medali nchini Morocco,” alisema Bagire siku moja kabla timu haijaondoka kwenda Morocco.

Aliongeza kusema: “Wachezaji wangu wana uzoefu mkubwa wa mashindano ya kimataifa ambao nina uhakika utatuongoza sisi katika ushindi. Tutacheza dhidi ya baadhi ya wachezaji bora Afrika lakini sisi ni mabingwa watetezi wa Para Taekwondo na tunatakiwa kuonesha kuwa ushindi wetu wa mwaka jana hatukubahatisha.

Ikishika nafasi ya nane katika ubora wa mchezo huo Afrika, kwa mujibu wa Shirikisho la Dunia la Taekwondo (WTF), Rwanda itakuwa ikisaka mafanikio ya kutetea taji lao la Afrika walioutwaa mwaka jana mjini hapa.

Katika mashindano hayo ya Afrika, Rwanda itakuwa na timu iliyokamilika ya wachezaji 14, nane katika taekwondo na sita katika Para Taekwondo. Wapambanaji wa Rwanda watakutana na ushindani mkali kutoka kwa wenyeji Morocco, Misri, Algeria, Tunisia na Gabon.

Timu kamili: Para Taekwondo: Jean de la Croix Nikwigize, Consolee Rukundo, Jean Claude Niringiyimana, Jean Marie Vianney Bizumuremyi, Parfait Hakizimana na Jean Pierre Manirakiza Taekwondo: Benoit Kayitare (captain), Savio Nizeyimana, Vincent Munyakazi, Moussa Twizeymana, Delphine Uwababyeyi, Raissa Umurerwa, Aline Ndacyayisenga na Benise Uwase.

Source:habarileo

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here