Ronaldo Anataka Mshahara Mkubwa Kuliko Messi

0
4

Taarifa zinaelezwa kuwa nyota wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo anaweza akawa mchezaji anayelipwa zaidi kuliko mpinzani wake wa FC. Barcelona, Lionel Messi. Imeripotiwa kuwa Real Madrid wameshaanza mazungumzo na mchezaji huyo ya kuongeza mkataba huku Ronaldo akitaka alipwe mshahara wa euro €1m kwa wiki.

 Mabosi wa Real Madrid wamefurahishwa na kiwango cha mchezaji huyo ambaye ameonesha kupanda kiwango chake baada ya kufunga jumla ya mabao 21 katika michezo 13 aliyocheza msimu huu. Kwa mujibu wa jarida la The Marca kutoka Spain, limeeleza Messi analipwa kitita cha €46m huku Ronaldo akilipwa €21m hivi sasa. Kama Ronaldo akiongeza mkataba wake basi amehitaji mshara wake upande zaidi ya Messi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here