Q Boy: Sina bifu na WCB

0
2
NYOTA wa Bongo Fleva, Q Boy Msafi, amesema yupo tayari kufanya kazi na msanii yeyote wa lebo ya WCB iliyopo chini ya Diamond Platinumz na wala hana bifu nao licha ya kwamba alitimuliwa kundini humo mwaka jana.
Q Boy alikuwa chini ya Diamond lakini baadaye walishindwana na akatimuliwa lakini mwenyewe amedai kuwa yupo tayari kuendelea kushirikiana na wakali wa kundi hilo akiwemo bosi wake huyo wa zamani.
“Nimefanya kazi na wasanii kadhaa bongo na nje pia, kama ikitokea kuna kazi ya kufanya na msanii wa WCB basi nitafanya tu kwani ninachoangalia zaidi ni maslahi yangu,” alisema Qboy Msafi ambaye pia ni mbunifu wa mavazi.

Na Vicent Segona vicent@spoti.co.tz

Source: Mwanaspoti

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here