PSG yamtolea macho Antonio Conte

0
3
  • Conte aliweka heshima baada ya kuipatia Chelsea taji katika msimu wake wa kwanza  ambapo hivi sasa wamekuwa nyuma kwa pointio 25 dhidi ya kinara Man City.
Klabu ya PSG imeanzisha mazungumzo na Kocha wa Chelsea, Antonio Conte kupitia wawakilishi wake ambapo anatajwa kumrithi Unai Emery ambaye anakaribia kutimkia kikosini hapo.
PSG inaonekana kukoleza moto wa kumchukua kocha huyo baada ya kutokuwapo na uwezekano wa Conte kwenda kuifundisha timu yake ya Taifa ya Italia.
Kwa sasa vita ya nani atakuwa kocha wa Italia imehamia kwa Roberto Mancini na Carlo Ancelotti.
Suala la Conte kuinoa PSG inaonekana kupewa kipaumbele zaidi kuliko kocha mwingine yeyote barani Ulaya.
Conte aliweka heshima baada ya kuipatia Chelsea taji katika msimu wake wa kwanza  ambapo hivi sasa wamekuwa nyuma kwa pointio 25 dhidi ya kinara Man City.
Majeraha mengine yanayoikabili Chelsea ni kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya katika hatua ya 16 bora baada ya kuondolewa na wababe wa Hispania, Barcelona.
Taarifa zinaeleza kuwa Emery anatarajiwa kuondoaka PSG baada ya mkataba wake kumaliziaka mwishoni mwa msimu huu.

Na Mwandishi wetu: Richard Mlelwa /barua pepe mlelwa@spoti.co.tz

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here