Niyonzima Aanza Mazoezi Ya Uwanjani, Baada Ya Ajali Ya Pikipiki, Mbonde Sasa Safi.

0
11

Baada ya ajali ya pikipiki, beki Salim Mbonde wa Simba ameanza mazoezi na wenzake.
Hata hivyo, Mbonde amekuwa akizunguka uwanja pembeni kuhakikisha anakuwa fiti kabla ya kuungana na wenzake.
Pamoja na Mbonde, kiungo Haruna Niyonzima ambaye alikuwa ameingia kwenye hofu huenda ya kukosa msimu mzima, naye ameanza mazoezi ya uwanjani.
Niyonzima alisafiri hadi India ambako alipatiwa matibabu ambaye yameondoa hofu ya kuukosa msimu hadi mwisho na sasa ameanza mazoezi ya uwanjani lakini kwa kuzunguka pembeni ya uwanja.
Niyonzima na Mbonde walikuwa wakizunguka uwanja wakati Simba ikijifua leo jioni kwenye Uwanja wa Boko Veterani jijini Dar es Salaam.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here