Ndoto ya Simba yafia Misri

0
4
Ndoto ya Simba yafia Misri

Port Said, Misri. Ndoto ya Simba kurudi kwa kishindo katika mashindano ya kimataifa imezimika baada ya kulazimisha suluhu na Al Masry.
Vinara hao wa Ligi Kuu, Simba waliingia katika mchezo huo wakitakiwa kushinda baada ya mchezo wa kwanza kulazimishwa sare 2-2 nyumbani hivyo ni ushindi pekee uliotakiwa kuwabeba ilikusonga mbele.
Kuondolewa huko kwa Simba katika mashindano hayo kutawalazimisha kupambana vilivyo kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Bara ili msimu ujao wacheze tena mashindano ya kimataifa.
Simba inayolingana pointi na Yanga katika msimamo wa Ligi Kuu iwapo watashindwa kutwaa ubingwa huo msimu huu basi watawashudia watani zao Yanga au Azam wakiwakilisha Tanzania katika mashindano hayo makubwa kwa klabu barani Afrika.
Al Masry ilianza mchezo huo kwa kasi kubwa na kufanya mashambulizi matatu makali katika dakika tatu za mwanzo lakini kipa wa Simba, Aishi Manula alikuwa imara na kuokoa zote.
Simba ilicheza kwa kujihami na kupoozesha mchezo na kwenye dakika ya 14 kiungo wa Al Masry, Farid Eman aliumia na nafasi yake kuchukuliwa na Aristide Bance.
Manula aliibuka tena shujaa katika dakika ya 20 baada ya kuokoa shambulizi la hatari la wenyeji hao lakini aliumia na kulazimika kufanyiwa matibabu kwa dakika mbili.
Simba ilinyanyuka na kupanda kushambulia katika dakika ya 22 ambapo shuti la Mganda, Emmanuel Okwi lilikwenda nje kidogo ya lango.
Al Masry ilifanya mashambulizi mengine mawili katika dakika ya 25 na 27, lakini Manula alikuwa imara na kuokoa kabla ya falo ya Nicholas Gyan kudakwa na kipa wa Al Masry dakika moja baadaye.
Mshambuliaji raia wa Bukinafaso, Bance alitaka kuchafua hali ya hewa katika dakika ya 37, lakini shuti lake kali lilidakwa na Manula.
Tafrani ilitokea katika dakika ya 43 baada ya beki wa Simba, Yusuf Mlipili kugongana na mchezaji mmoja wa Al Masry na kupelekea mchezo kusimama kwa dakika tatu ila upande ukidai kuwa ndio umefanyiwa faulo. Hata hivyo mwamuzi aliamuru fualo ipigwe kwenda Simba lakini haikuwa na madhara.
Kipindi cha kwanza kilimalizika bila timu yoyote kupata bao a A Masry walirejea kipindi cha pili kwa kasi na kufanya mashambulizi matatu makali katika dakika 10 za mwanzo lakini hayakuwa na madhara makubwa kwa Sima kutokana na uimara wa safu ya ulinzi.
Gyan alipoteza nafasi ya kuifungia Simba bao la utangulizi katika dakika ya 55 lakini shuti lake lilipaa juu kidogo ya lango.
Simba ilipoteza tena nafasi adhimu katika dakika ya 60 baada ya shuti la Kwasi kupaa juu kidogo ya lango na dakika nne baadaye straika Mrundi, Laudit Mavugo aliingia kuchukua nafasi ya Mlipili.
Simba iliamka na kuanza kutengeneza mashambulizi jambo ambalo lilimpa hamasa kocha Mfaransa, Pierre Lechantre ambaye alimtoa tena kiungo, James Kotei na kumpa nafasi, Shiza Kichuya katika dakika ya 74.
Mavugo alipoteza nafasi ya dhahabu ya kuipatia Simba bao la utangulizi katika dakika ya 79 baada ya shti lake kali kudakwa na kipa wa Al Masry.
Kutokana na kasi ya mchezo huo nyota wa Simba, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Juuko Murshid na John Bocco walionyeshwa kadi za njano katika vipindi vyote viwili.
Baada ya kuona Simba imeongeza kasi ya mashambulizi Al Masry iliamua kuanza kupoteza muda ambapo wachezaji wake walijiangusha katika dakika tano za mwisho za mchezo huo.
Kabla ya mchezo
Hali ilikuwa tafrani kabla ya mchezo kuanza ambapo kwanza Simba iligomea basi ililopewa na Al Masry na kupanda jingine jambo ambalo lilipelekea maofisa wa timu hiyo kupaniki na kulizua.
Kigogo wa Simba, Musley Ruwey anayezungumza Kiarabu alikomaa na Waarabu hao mpaka baadaye wakakubali litumike basi lililochaguliwa na Simba.
Kabla ya kuanza kwa mchezo maofisa wa All Masry waliingia na njiwa uwanjani na kuzifungulia juu ikiwa ni ishara ya imani za miungu mingine.
Wakati wa mapumziko afisa mmoja wa Al Masry aliingia uwanjani na kumwaga maji kwenye goli la Simba huku akisali lakini imani hizo haba hazikuweza kuzaa matunda.
Source: Mwanaspoti

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here