Msimbazi wakate wenyewe tu

0
7
MAMBO ni moto kweli kweli. Nyota wa zamani wa Simba, wameingilia kati kuhakikisha timu hiyo inatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu, wakisema nguvu iliotumika kukiandaa kikosi dhidi ya Al Masry ndiyo itumike kumalizia mechi zilizobakia.
Simba imekabwa koo na Yanga kileleni mwa ligi zote zikiwa na pointi 46, japokuwa Wana Msimbazi wanaongoza kwa wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Nahodha wa zamani wa timu hiyo, Masoud Nassor ‘Chollo’ amesema soka waliloonyesha Simba dhidi ya Al Masry katika Kombe la Shirikisho, linapaswa kuendelezwa katika ligi.
“Mimi ni mchezaji, najua kitu kilichowafanya waupige mpira mwingi kule Misri, mfano mzuri ni maandalizi yanayofanywa Simba ikicheza na Yanga, viongozi wanakuwa karibu na wachezaji kuhakikisha wanakuwa watulivu, wanatatua shida zao na ndicho kitakachowafanya watwae ubingwa msimu huu, wasibague mechi,” alisema.
Danny Mrwanda, ambaye aliyeichezea timu hiyo kwa nyakati tofauti, alisema kufanana pointi na Yanga si mwisho wa ndoto zao, ila viongozi na benchi la ufundi watumie hekima ya hali ya juu kuongoza jahazi hilo.
“Bado Simba wana nafasi ya ubingwa, kinachotakiwa ni busara za viongozi kwa wachezaji wanaowategemea walete taji hilo, katika mechi zilizosalia,” alisema.
Chanzo: Mwanaspoti

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here