Mourinho ampa makavu Pogba

0
4

KOCHA wa Manchester United, Jose Mourinho yamemfika, kakosa uvumili na ameshatangaza hadharani hamtaki kikosini mwake Paul Pogba na anayemtaka aweke mzigo mezani wakubaliane.

Kuonyesha kweli hana mpango naye tena, Mourinho ameshaanza kumkomalia

Toni Kroos kama mbadala wake.

Manchester United ilivunja rekodi ya uhamisho wa Pogba mwaka 2016 kwa kumrudisha mchezaji huyo Old Trafford, lakini sasa mambo yamegeuka, Mourinho hamtaki kutokana na tabia yake.

Pogba ameanza mechi nne kati ya 11 na aliachwa kwenye kikosi kilichoanza katika mechi ya FA Cup waliyoshinda dhidi ya Brighton.

Lakini kuna ripoti zinasema kuwa Mourinho alianza kukertwa na vijitabia vya Pogba hasa katika mchezo wa Liverpool, mechi ambayo Pogba hakucheza kwa kuwa alikuwa majeruhi.

Mourinho sasa akili yake ni kwa Mjerumani, Kroos ambaye miaka minne iliyopita alikaribia kutua Old Trafford lakini baadaye akaghairi na kwenda zake Real Madrid kwa dau la Pauni 24 milioni akitokea Bayern Munich wakati huo alikuwa amebakisha mwaka mmoja wa mkataba wake kumalizika.

Chanzo:Mwanaspoti.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here