Model wa video ya ‘Ntampata Wapi’ ya Diamond ashinda taji la Top Model SA

0
3

Mrembo huyo aitwaye  Melissa Magiera ambaye kwa sasa yupo chini ya kampuni ya Fan Jam Model Management, wiki iliyopita amefanikiwa kushinda taji la Top Model 2018 nchini Afrika Kusini.

Melissa ameshinda taji hilo kwa kuwabwaga washiriki wengine 38 ambao walifanikiwa kutinga katika hatua ya nusu fainali.
Mrembo huyo ataiwakilisha Afrika Kusini kwenye mashindano ya Top Model ya dunia ambayo yatafanyika Ijumaa ya April 6 na 7 ya mwaka huu mjini London.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here