Mchezaji afariki dunia kwa kutuliza mpira kifuani

0
4

Croatia. Mchezaji soka Bruno Boban amefariki baada ya kutuliza mpira kifuani wakati wa mechi.
Mchezaji Boban alituliza shuti lililopigwa na mwenzake kifuani wakati wa mechi kati ya Marsonia dhidi ya Slavonija Pozega katika mchezo wa Ligi Daraja la Tatu Croatia.

Mchezaji huyo mwenye miaka 25, alionekana yuko salama, lakini dakika chache baadaye alidondoka na kupoteza fahamu uwanjani.

Wachezaji wenzake na madaktari walijaribu kumuokoa Boban kwa kumpa huduma ya kwanza.
Madaktari walijaribu kumsaidia mchezaji huyo kwa dakika 40, lakini hawakufanikiwa.

Boban alitangazwa amepoteza maisha uwanjani hapo, japokuwa chanzo cha kifo chake bado hakitangazwa.
Timu yake Boban ilitumia ukurasi wao wa Facebook, kutoa pole kwa familia yake kwa kwa kumpoteza kijana wao.
Chanzo:Mwanaspoti

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here