Mbwana Samatta Ameshatua Algeria Kuungana Na Wenzake Wa Taifa Stars

0
10
Mara baada ya msafara wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kuondoka Dar es Salaam kwenda Algeria, jana Jumatatu, mshambuliaji Mtanzania, Mbwana Samatta tayari ameshatua nchini humo kuungana na wenzake hao.
Samatta aliwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Algiers, Algeria, na kupokelewa na Balozi wa Tanzania nchini humo, Omar Yusuph Mzee.
Staa huyo amewasili Algeria kwa ajili ya mchezo huo wa kirafiki, ambapo Taifa Stars itacheza dhidi ya Algeria mnamo Machi 22 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here