Mbonde Na Niyonzima Kurejea Kesho

0
8
Kikosi cha Simba Sc kesho siku ya Jumamosi march 24  kinarejea mazoezini kujiandaa na michezo za ligi kuu dhidi ya Njombe April 03 katika uwanja wa Sabasaba na dhidi ya Mtibwa April 08 katika dimba la jamhuri Morogoro.
Majeruhi wa kikosi hicho Salim Mbode ambaye hivi karibuni kabla ya kwenda Kikosi kwenda Misri alipata ajari ya Pikipiki na kupelekea kushonwa nyuzi tatu kwenye jicho na nyuzi zimeondolewa na sasa yuko tayari kurejea uwanjani.
Kabla ya kupata ajali Mbonde alikuwa majeruhi kwa miezi 4 na nusu aliporejea akawa fiti na akawa kwenye  orodha ya wachezaji ambao wangeenda Misri kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya Al masry ila akapata ajari siku moja kabla ya safari.Pia Kiungo Haruna Niyonzima naye kesho anarejea kwenye mazoezi ya klabu hiyo ila atakuwa chini ya ungalizi  maalumu wa kocha wa Viungo Mohammed Habibi na Daktari wa Timu hiyo Yassin Gembe. 
Niyonzima naye amekaa nje ya uwanja kwa muda wa miezi 4 akiuguza majeraha katika mguu wake mara ya mwisho Haruna Niyonzima kuitumikia klabu ya Simba ilikuwa November 26 mechi ya VPL dhidi ya Lipuli tangu hapo hajawahi kucheza mechi yoyote.
-Niyonziwa alikuwa afanyiwe oparesheni kwenye jeraha lake ila alienda India kufanyiwa matibabu na akaambiwa atatibiwa kwa njia nyingine ambayo sio ya oparesheni na sasa amefanya mazoezi binafsi ya ufukweni kujiweka fiti na sasa anarejea kufanya mazoezi na kikosi cha Simba chini ya uangalizi maalumu.
@yossima Sitta Jr.
Imeletwa na: Agape Patrick
   Email: agape@spoti.co.tz

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here