Lipuli mechi moja tu wamebaki

0
2
MIPANGO inazidi kusukwa kwenye kikosi cha Lipuli a.k.a Wana Paluhengo ili kuhakikisha wanasalia Ligi Kuu Bara.
Hiyo ni baada ya Kocha Mkuu wa Lipuli, Amri Said, kusema wanapambana kuhakikisha wanashinda mechi zote zilizobaki ili kukaa pazuri. Lakini, winga wa klabu hiyo, Jamal Mnyate, amesema kikosi chao kinahitaji pointi tatu ili kubaki katika ligi na baada ya hapo watasaka kumaliza nafasi za juu.
Alisema kwa pointi 27 walizonazo sasa, wakishinda mechi moja watakuwa na 30 zitakazowafanya wasishuke na badala yake itakuwa ni kutafuta ubora na si kumaliza ligi kwa udhaifu.
“Sema kwa mfumo wetu wa ligi ulivyokaa ni ngumu kupanda, lakini ingekuwa Ulaya kwa nafasi tuliopo tungeweza kuchukua ubingwa, tofauti na sasa ukisema Lipuli tutachukua ubingwa wataona ni ndoto za mchana,” alisema.
Naye straika wa timu hiyo, Malimi Busungu alisema kikosi chao kina uwezo wa kumaliza nafasi za juu, kinachotakiwa ni kujiamini na kuelekeza nguvu kwenye malengo yao.
Chanzo: Mwanaspoti

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here