Kocha wa Simba atimkia Ufaransa

0
9
Misri.  SIMBA inalazimika kurejea jijini Dar es Salaam bila kocha wake mkuu, Mfaransa Pierre Lechante ambaye ameomba likizo fupi kwenda kwao Paris.
Lechantre aliiongoza Simba kupata suluhu dhidi ya Al Masry ya mjini hapa jana Jumamosi lakini timu hiyo iliondoshwa kwenye mashindano hayo ya kombe la Shirikisho Afrika kwa faida ya bao la ugenini kufuatia sare ya mabao 2-2 nyumbani.
Simba imemkatia tiketi ya ndege kwenda kwao Paris leo Jumapili na anatarajiwa kurejea Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Wakati huohuo, nyota wa Simba wamepewa mapumziko ya siku tano ili kujiweka sawa kabla ya kuanza kujifua upya kwaajili ya mechi za Ligi Kuu Bara.
Simba itaondoka mjini hapa Alfajiri ya kesho na inatarajiwa kuwasili Dar es Salaam majira ya mchana kwa Shirika la Ndege la Ethiopia.
Source: Mwanaspoti

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here