Kocha Majimaji : Hakuna Kulala Kazi Juu Ya Kazi Mpaka Kieleweke.

0
4
Kutokana na mwenendo mbaya katika Ligi Kuu ya Vodacom, mambo ndani ya Majimaji siyo mazuri na hiyo imesababisha kikosi cha timu hiyo kuendelea kufanya mazoezi na kutokuwa na muda wa mapumziko.

Hadi sasa Majimaji inashika nafasi ya chini katika msimamo wa ligi hiyo.
Ofisa Habari wa Majimaji, Onesmo Ndunguru amethibitisha juu ya taarifa hizo kwa kusema kuwa benchi la ufundi chini ya Kocha Mkuu Habib Kondo limeamua timu hiyo haitakuwa na muda wa kupumzika.
Wakati huu mapumziko ya ligi hiyo kupisha ratiba ya timu ya taifa na michuano ya kimataofa wachezaji wa timu hiyo wamekuwa wakiendelea na mazoezi.
Alisema kulingana na nafasi walikuwepo katika msimamo wa ligi hiyo, ameamua kufanya hivyo ili kuendelea mazoezi kwa ajili ya kujiweka fiti na kuongeza wachezaji vijana kutoka kikosi B kutia nguvu ndani ya timu hiyo.
Chanzo: BINZUBEIRY

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here