Kimwaga wa Azam aibuka kwa kishindo

0
3

Winga wa Azam FC, Joseph Kimwaga ambaye amekaa nje ya uwanja kwa zaidi ya nusu mwaka akiuguza majeraha hatimaye amerejea dimbani kwa kishindo baada ya kutumia dakika 7 kufunga mabao mawili.

Kimwaga amefunga mabao hayo kwenye mchezo wa kirafiki jana usiku wakati timu yake ya Azam FC ilipoichapa Friends Rangers mabao 5-0 kwenye uwanja wa Azam Complex, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo wa kombe la shirikisho.
Kimwaga aliingia kipindi cha pili ikiwa ni mchezo wake wa kwanza tangu apate kibali cha daktari cha kuanza kucheza, alifunga mabao hayo katika dakika ya 75 na 82 ambayo yalihitimisha ushindi huo mnono.
Baada ya mchezo huo wa jana, kikosi cha Azam FC leo kimepumzishwa na kitarejea tena mazoezini Jumatatu ijayo jioni kumalizia maandalizi ya kuikabili Mtibwa Sugar katika mchezo wa Kombe la Shirikisho nchini (ASFC).
Kimwaga amekaa nje kwa miezi nane akiuguza majeraha ya goti. Ametibiwa katika hospitali moja nchini Afrika Kusini chini ya jopo la madaktari wa huko pamoja na daktari wa Azam FC.
Chanzo:EATv

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here