JULIO: Sio Rahisi Ubingwa Kutua Simba

0
3

Kocha wa Dodoma FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema Simba ina kibarua kigumu katika mbio za ubingwa msimu huu kutokana na ugumu wa mechi wanazokabiliana nazo.
Simba ipo kileleni kwa idadi ya mabao ya kufunga ikiwa pointi sawa na Yanga huku wakiwa na mchezo mmoja mkononi dhidi ya Njombe Mji.

“Simba walikuwa juu kwa pointi nane msimu uliopita na Yanga wakawa mabingwa, msimu huu walitangulia kwa pointi saba lakini wamefikiwa, hata kama wana mchezo mmoja mkononi haijalishi, watu wanasema ni bora ulichonacho kuliko unachokitegemea ambacho unaweza usikipate.
“Huwezi kusema Simba wanaweza kuwa mabingwa ingawa wana timu nzuri, wana mechi nyingi ngumu hapo katikati ikiwemo na ya Yanga wenyewe, kwenye mpira lolote linaweza kutokea,” alisema Julio.
Na Agape Patrick
Email  agape@spoti.co.tz
Chanzo: Global Publishers

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here