Hukumu ya kifungo cha maisha, Wambura akata rufaa

0
4

Wakili wa makamu wa Rais wa Shirikisho la soka nchini Emmanuel Muga, amethibitisha kukamilisha taratibu zote za kumkatia rufaa mteja wake Michael Richard Wambura ili shauri lake liweze kusikilizwa tena.
Muga amesema katika rufaa hiyo wamewasilisha mambo matano ambayo wameomba yasikilizwe kwa hati ya dharula kwani mteja wake (Michael Richard Wambura) ni mtu mwenye majukumu mengi ya kitaifa na kimataifa.
“Rufaa hiyo tumeomba isikilizwe kwa hati ya dharula kwa sababu Wambura ni kamishna wa mechi wa shirikisho la soka Afrika na mwezi ujao ameteuliwa kuwa kamishna kwenye mechi ya Rwanda na Kenya, lakini pia ni kiongozi wa mkoa na kitaifa pia,” Muga ameeleza.
Muga ambaye aliwahi kuwa mwanasheria wa TFF siku za nyuma amesema miongoni mwa mambo waliyoyakatia rufaa ni kuhoji uhalali wa kamati iliyomtia hatiani mteja wake ambapo kikanuni haina mamlaka ya kufanya maamuzi hayo.
“Moja wapo ya sababu ya rufaa ni kuwa kamati haikuwa na mamlaka ya kufanya walichokifanya, sababu nyingine kamati haikufuata sheria na katiba ya TFF wakati inafanya maamuzi, pia kamati haikumpa Wambura nafasi ya kusikilizwa na pia kamati hakupokea ushahidi wowote walijiamulia tu,” Muga amesema.
Makosa yake
Ikumbukwe kuwa mchana wa Machi 15, 2018 Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka nchini (TFF), ilimfungia maisha kutojihusisha na shughuli za soka Makamu wa Rais wa TFF, Michael Wambura.
Inadaiwa kuwa Wambura amefungiwa kutokana na kupokea fedha zisizo halali kiasi cha Shilingi milioni 84, pamoja kughushi nyaraka za malipo, na kula njama kulipwa fedha na waliokua viongozi wa TFF Jamal Malinzi na Selestin Mwesigwa.
Source: FUTAA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here