Hii ndio mikakati ya Taifa Stars

0
4
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya soka ya Tanzania Taifa Stars Salum Mayanga, ameweka wazi mikakati ya mazoezi ya timu hiyo kuelekea mchezo wa kirafiki dhidi ya DR Congo jumanne ijayo.
Mayanga amesema baada ya jana timu hiyo kuwasili nchini ikitokea Algeria na kupata mapumziko ya masaa kadhaa, leo asubuhi imeanza mazoezi mepesi kwaajili ya kurejesha afya kwenye hali nzuri baada ya mchezo uliopita na uchivu wa safari.
Mtaalam huyo wa ufundi ambaye mkataba wake wa kufundisha timu hiyo umemalizika, ameeleza baada ya mazoezi ya asubuhi timu itapumzika na jioni itaanza rasmi mazoezi kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
Programu hiyo ya mazoezi itaendelea kesho jumatatu ambapo asubuhi timu hiyo itafanya mazoezi ya mwisho kabla ya mchezo huo wa jumanne ambao ni wa pili kwa kalenda ya FIFA kwa mwezi Machi baada ya kukubali kipigo cha mabao 4-1 kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Algeria.
Aidha Mayanga amesema mechi za mwezi huu ni kipimo sahihi kwa Stars kutokana na viwango vya timu hizo kuwa juu kwenye orodha ya timu wanachama wa FIFA ukilinganisha na timu zingine ambazo wamecheza nazo huko nyuma.

Chanzo:EATv

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here