Heee! Mourinho na Pogba hawaongei (Bifu)

0
4


Imeripotiwa kuwa mahusiano ya kiungo wa Manchester United, Mfaransa, Paul Pogba na Kocha wake Jose Mourinho si mazuri.Kwa mujibu wa Daily Star limeandika kuwa wawili hao hivi sasa hawazungumzi, na badala yake mawasiliano kati ya wawili hao yanapitia kwa Kocha Msaidizi, Rui Faria.Taarifa za Pogba na Mourinho kutokuwa na mawasiliano mazuri zimezidi kuteka vyombo vya habari kwa muda mrefu sasa.Sababu kubwa ya suala hili kufikia hatua hii ni Kocha Mourinho kushindwa kumtumia Pogba katika kikosi kwa siku za hivi karibuni.Siku kadhaa zilizopita Pogba alisema anatamani siku moja acheze soka sambamba na Neymar Junior anayeichezea PSG ya Ufaransa. Dalili zinaonesha kabisa anaweza akaachana na Manchester United.Source: Saleh Jembe
Imeletwa na agape patrick
Email: agaoe@spoti.co.tz

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here