Hawa ndio wapinzani wa Yanga walivyo wajue kiundani..

0
8

HAWA NDIO WOLAYTA DICHA SC WAPINZANI WA YANGA SHIRIKISHO Na Samuel Samuel Droo ya michuano ya kombe la Shirikisho Afrika hatua ya mtoano imefanyika usiku huu wa tarehe 21 Machi 2018 na mabingwa wa kihistoria nchini Yanga SC kuangukia mikononi mwa wahabeshi Wolayta Dicha SC toka nchini Ethiopia. Wolayta ni moja ya timu changa katika historia ya soka la Afrika lakini yenye mrengo mzuri wa mafanikio kutokana na mipango yao toka kuanzishwa kwao mwaka 2009 hii ni tofauti na wapinzani wao Yanga SC walioanzishwa Februari 11, 1935. Mwaka 2009 wakazi wa jimbo la Wolayta Sodo kusini kati mwa nchi ya Ethiopia pembezoni mwa mto maarufu uitwao Omo, waliamua kuanzisha timu yao ya soka kutoka jamii ya wakulima kwa ajili ya kupata ushiriki wa ligi kuu ya nchi hiyo. Sodo ni moja ya miji inayokuwa kwa kasi hivi sasa nchini Ethiopia ukiachia vurugu za kisiasa hivyo kuwa na timu imara ni jambo ambalo lilikuwa kiu ya wanazi wa soka mjini humo ingawa kijiografia timu hii inatokea katika mji wa Hawasa uliopo ndani ya bonde la Ufa pembezoni mwa ziwa ambalo linapokea maji ya mto Omo. Hivyo ndivyo ilivyoanzishwa hii timu na mwaka 2013-14 kwa mara ya kwanza ikafanikiwa kushiriki ligi kuu ya nchi hiyo. Wolayta inayoundwa na wazawa kwa sehemu kubwa ikiwa na nyota wao Mubarek Shukur , iliwachukua miaka minne tu kabla ya kutawazwa mabingwa wa ligi kuu nchini Ethiopia baada ya kuibuka mabingwa msimu wa 2016-17 ikiwa ni mara yao ya kwanza katika historia yao. Ubingwa huo ndio uliowapa tiketi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa Afrika wakiianza karata yao nchini Tanzania dhidi ya Zimamoto ya Unguja na kutoka sare ya 1-1 na wakafanikiwa kuingia 16 bora baada ya kupata ushindi mwembamba wa goli 1-0 nyumbani kwa jumla ya magoli 2-1.Hatua ya 16 bora Wolayta walikutana na vigogo wa Afrika timu ya Zamaleki mabingwa mara tano klabu bingwa Afrika na kutolewa kwa mikwaju ya penati ya 3-4. Mjini Hawasa Wolayta walishinda 2-1 na Zamaleki pia wakashinda 2-1 jijini Cairo na kuifanya mechi kusimama kwa aggregate ya 2-2 kitu ambacho kilipelekea mikwaju ya penati na Zamaleki bahati kuangukia upande wao kwa kushinda 4-3.Licha ya uchanga wao lakini kitendo cha kumsumbua Zamaleki katika kuitafuta tiketi ya hatua ya makundi klabu bingwa , wanatoa salama za hatari kwa Yanga SC kujiandaa vyema dhidi ya nyuki hao wa Ethiopia. Nyuki ndio jina lao la utani. Historia kisoka, ukongwe na idadi ya vikombe ilivyonavyo Yanga SC inaizidi mbali sana timu hii lakini ni moja ya timu ngumu kutokana na soka lao la kasi , nguvu na moyo wa kushindana kwa dakika zote 90. Ni timu yenye kiu ya kuingia kwenye ramani ya soka la Afrika hivyo Yanga inawapasa kuchukua tahadhari kubwa kutoipa nafasi timu hii kuandika historia hiyo kupitia wao kama walivyofanya kwa Township Rollers. Ukiondoa wazawa ina wachezaji watatu toka Ufaransa, Nigeria na Liberia hivyo ni timu ambayo ina malengo na mikakati ya kufika mbali kisoka. Kufanikiwa kunyakua ubingwa wa ligi kuu ya Ethiopia na kuwachachafya Zamaleki kumewapa mashabiki wengi nchini kwao na kutengeneza ‘ tensioni ‘ Afrika. Asanteni. By Mchambuzi kipenzi cha wengi *Samuel Samuel* Source:Samuel Samuel         Imeletwa na:Agape patrick Email:agapepatrick1@gmail.com

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here