Dulla Mbabe atamba kummaliza Mwakyembe

0
9

BONDIA wa ngumi za kulipwa Abdallah Pazi ‘Dulla Mbabe’ ametamba kummaliza mpinzani wake mapema kwa ‘knockout’ Benson Mwakyembe katika pambano la ubingwa wa Afrika Mashariki litakalopigwa Aprili 6, mwaka huu.

Pambano hilo la raundi 12 litapigwa kwenye uwanja wa Kinesi Dar es Salaam ambapo Pazi atakuwa anautetea mkanda alioutwaa Februari baada ya kumchapa Mmalawi, Felix Mwamaso.

Akizungumza na gazeti hili jana Pazi alisema anaendelea na mazoezi kwenye ‘Gym’ na tayari ameshamchunguza mpinzani wake na kujua ana jeraha hivyo, mapema atamaliza mchezo huo.

“Najua Mwekyembe ni bondia mkongwe ila hanitishi zaidi nimejipanga kumkabili na nina uhakika wa asilimia 95 nitatetea mkanda wa Afrika Mashariki,” alisema.

Alisema muhimu ni mashabiki wa mchezo huo kujitokeza na kuwaunga mkono kushuhudia bondia bora akimmaliza mpinzani wake mapema. Bondia huyo alisema anahitaji kushinda ili kuendelea kutengeneza rekodi bora na kuvutia mialiko mingi ya nje.

Pazi anashika nafasi ya kwanza Tanzania kutokana na viwango vya ubora vya Boxrec huku akishika nafasi ya 140 duniani kati ya mabondia 1,351 kwa uzito wa Supermiddle Weight na mpinzani wake, Mwakyembe anashika nafasi ya pili Tanzania katika uzito wa Light Heavyweight na nafasi ya 263 duniani kati ya mabondia 1,105.

Mbali na hao, wengine watakaopanda jukwaa moja ni Mfaume Mfaume atakayechuana dhidi ya Habibu Pengo ‘Bad Face’, mkongwe Mada Maugo akipambana dhidi ya Kanda Kabongo na Francis Miyeyusho dhidi ya mpinzani atakayetajwa baadaye

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here