Diamond, Vanessa na Navy Kenzo wapongezwa na Damian Soul, kisa?

0
3

Msanii wa muziki Bongo, Damian Soul amelipongeza kundi la muziki la Navy Kenzo kwa kusema kuwa lilionyesha mwanga kwa wasanii wakubwa kuanza kutoa albamu.

Muimbaji huyo ambaye anafaya vizuri na ngoma ‘Data’ amesema wasanii walio mainstream waliacha kutoa albamu kwa kipindi fulani lakini baada ya Navy Kenzo kutoa na wengine wakafuata.
“Nadhani muamko ulioletwa na kama Navy Kenzo kwa sababu wao ndio waliotutoa kimasomaso kujaribu kwamba i want to do this kwa hiyo ilileta muamko kwa sababu wapo kwenye sportlight,” Damian ameiambiaBongo5.
“So we thanks God for Vanessa, Navy Kenzo lakini tunashukuru kwa Wakazi pia kwa Diamond as well wamekuwa mfano na sisi wengine tutafuata kwa sababu tunataka industry yetu iwe pale juu,” amesisitiza.
Hata hivyo ameongeza kuwa si kwamba wasanii walikuwa hawatoi albamu kabisa ila kuna ambao walitoa lakini hawakupewa kipaumbele kama wanachopewa wanaotoa sasa huku akimtolea mfano One The Incredible kama miongoni mwa wasanii hao.

by richard@spoti.co.tz

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here