Congo Wapo Dar Es Salaam Kwa Ajili Ya Stars

0
5

Kikosi cha timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemorasia ya Congo ‘The Leopards’, kimewasili asubuhi ya leo jijini Dar es Salaam. Congo wamewasili kwa ajili ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki ulio kwa mujibu wa kalenda ya FIFA dhidi ya Taifa Stars. Mechi inatarajiwa kupigwa kesho kutwa Jumanne ya Machi 27 2018 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kikosi cha Stars nacho kiliwasili jana ikitokea nchini Algeria baada ya mechi yake dhidi ya taifa hilo kumalizika Alhamis ya wiki hii. Tayari viingilio vya mchezo huo vilishatajwa ambapo VIP A, B na C italipiwa kwa shilingi 5000 tu huku mzunguko ukilipiwa kwa shilingi 1000.
Chanzo:FullShangwe

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here