Yanga: Thamani ya Kazadi Kasengu ni milioni TZS 695.7

1 month ago 449

Kampuni ya Be Sports Management inayomsimamia mshambuliaji wa kimataifa wa DR Congo na klabu ya Al Masry ya Misri Francy Kazadi Kasengu imesema kuwa mshambuliaji huyo ni mchezaji halali wa klabu ya Al Masry sio Wydad Casablanca ya Morocco.

Kampuni hiyo imedai kuwa hakuna mazungumzo yoyote na klabu ya Yanga SC ya Tanzania kuhusu usajili wa nyota huyo ambaye ana mkataba na Al Masry mpaka June 2024. Pia ameongeza kuwa thamani ya Kazadi kwa sasa ni dola 300,000 (ambazo ni milioni 695.7 za Kitanzania)

Yanga ni klabu pekee nchini Tanzania imeonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji huyu hatari zaidi, Swali kubwa ni je Yanga wapo tayari kutoa kiasi hiki kikubwa cha fedha?