RONALDO APIGA MBILI MAN U YASHINDA 4-0

1 week ago 88

MSHAMBULIAJI Mreno, Cristiano Ronaldo amerejea kwa kishindo Manchester United baada ya kufunga mabao mawili dakika ya 45 na ushei na 62 katika ushindi wa 4-1 leo dhidi ya Newcastle United Uwanja wa Old Trafford.
Mabao mengine ya Man United yamefungwa na Bruno Fernandes dakika ya 80 na Jesse Lingard dakika ya 90 na ushei, wakati la kufutia machozi Newcastle United limefungwa na Javi Manquillo dakika ya 56.
Ushindi huo unaifanya Manchester United ifikishe pointi 10, moja zaidi ya mahasimu wao wa Jiji, Manchester City, Brighton & Hove Albion na Tottenham Hotspur, wakati Newcastle United inabaki na pointi moja baada ya wote kucheza mechi nne.