Rais wa TFF atuma salamu za rambirambi

1 week ago 66

Rais wa Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF), Wallace Karia amepokea kwa mshtuko msiba wa Mjumbe wa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya shirikisho hilo, Zakaria Hanspope aliyefariki jijini Dar es salaam katika Hospitali ya Aga Khan Jana Ijumaa (Septemba 10).

Karia amewasilisha salamu za rambirambi kwa famia ya Hanspope pamoja na wadau wa soka nchini kwa ujumla, ambao wanaendelea kuomboleza msiba wa kiongozi huyo, ambaye pia alikuwa mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba SC.

Wengine waliowasilisha salamu za rambirambi kufuatia msiba wa Hanpope:

Klabu ya Simba: Tumempoteza Mwanasimba wa kweli.
Pumzika kwa amani Hans Poppe. #RIPHansPoppe #NguvuMoja

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Mohammed Dewji: “Nimefanya kazi na wewe kwa miaka mingi, na kila siku uliweka maslahi ya Simba mbele.”

“Kaka yangu ulikua na wema wa kipekee, na ulikua wa kwanza na ulinyooka linapokuja suala la kuilinda Simba, hukuwa na maslahi binafsi. Ulikua rafiki wa marafiki wa Simba, na ulikua tofauti na wasioitakia mema Simba.”

Klabu ya Yanga: Uongozi wa Klabu ya Yanga umepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mjumbe wa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji TFF na Kiongozi wa Simba Sc, ndugu, Zacharia Hans Pope.

Tunatoa pole kwa Uongozi wa TFF, Simba Sc, Familia, Washabiki, Ndugu, Jamaa na Wanamichezo wote Nchini.

Klabu ya Azam FC: Poleni sana uongozi na mashabiki wa timu ya Simba kwa kuondokewa na mpendwa wenu, Zacharia Hans Poppe.

Haji Manara: “Nimechelewa sana kusikia taarifa za huu msiba wa mzee wetu Zacharia ,,,Imenifadhaisha sana na imeniondolea Mood yangu,,,,
Kwangu alikuwa Mwanamichezo halisi shupavu na ameacha pengo kubwa Kwa mpira wetu na klabu yake Kwa ujumla,,,
Pumzika Kwa amani Captain”

Gerson Msigwa ,MSEMAJI MKUU WA SERIKALI: Nimeshtushwa sana na kifo cha Ndugu Zacharia HansPope. Tumepoteza mdau muhimu kwa soka la nchi yetu na mtu aliyetamani kuona Tanzania inakaa kwenye viwango vya kimataifa vya soka.

Poleni sana wanafamilia, uongozi wa Simba Sports Club] wachezaji, wapenzi na wanachama wa Simba Sports Club] wapenzi wa soka na wote walioguswa na msiba huu.

Mara ya mwisho niliwasiliana nae kwa kuchati nikimpa pole kwa maradhi yanayomkabili, alinijibu huku akiwa kwenye mashine ya oksijeni (mashine ya kumsaidia kupumua). Aliniambia “ugonjwa unatesa sana huu” na baadaye akasisitiza watu wachukue tahadhari.

Tumuombee apumzike mahali pema, tuwaombee wafiwa na tumuenzi kwa kuendeleza dhamira kubwa aliyekuwa nayo katika kuendeleza soka la Tanzania.

Mungu amweke mahali pema peponi, Amina.