MWENYEKITI WA WAZEE YANGA AFARIKI DUNIA

1 week ago 119


MWENYEKITI wa Baraza la Wazee la klabu ya Yanga, Hashim Muhika (pichani kushoto), amefariki dunia alfajiri ya leo Jumapili nyumbani kwake Mtoni Mtongani jijini Dar es Salaam.
Marehemu Muhika alifariki baada ya kuugua ugonjwa wa moyo kwa kipindi kirefu,  msiba wake upo Mtoni Mtongani.
Anatarajiwa kuzikwa kati ya makaburi ya maeneo matatu ya Kisiju, Mtoni Mtongani na Kisutu inaelezwa kikao kitakachokaliwa leo mchana majira ya saa 8, kitaamua.
Marehemu alifariki akiwa na umri wa miaka 87, ameacha mtoto mmoja na mjukuu mmoja.