MASHABIKI RUKSA YANGA NA RIVERS UNITED

1 week ago 77

 HATIMAYE Yanga SC imeruhusiwa kuingiza mashabiki katika mchezo wake dhidi ya Rivers United ya Nigeria.
Yanga SC watakuwa wenyeji wa Rivers United Jumapili Saa 11:00 jioni katika mechi ya kwanza ya Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam kabla ya timu hizo kurudiana Septemba 19 Uwanja wa Adokiye Amiesimaka Jijini Port Harcourt, Nigeria.
Na leo imetaja viingilio vya mechi hiyo ambavyo ni Sh. 30,000 VIP A, 20,000 VIP B, 10,000 VIP C na 5,000 kwa mzunguko.