CAF YAZUIA MASHABIKI MECHI YA YANGA

1 week ago 62


 SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limezuia watazamaji katika mechi ya kwanza Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika baina ya wenyeji, Yanga SC na Rivers United ya Nigeria kesho.
Kwa mujibu wa taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) leo, CAF imezuia watazamaji katika mechi zote za Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho na Ligi ya Mabingwa zinazochezwa Tanzania.
Yanga SC watakuwa wenyeji wa Rivers United kesho Saa 11:00 jioni katika mechi ya kwanza ya Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam kabla ya timu hizo kurudiana Septemba 19 Uwanja wa Adokiye Amiesimaka Jijini Port Harcourt, Nigeria.