BAYERN MUNICH YASHINDA 4-1 BUNDESLIGA

1 week ago 74

MABINGWA watetezi, Bayern Munich jana waliibuka na ushindi wa 4-1 dhidi ya wenyehji, RB Leipzig katika mchezo wa  Bundesliga Uwanja wa Red Bull Arena Jijini Leipzig.
Mabao ya Bayern Munich yalifungwa na Robert Lewandowski kwa penalti dakika ya 12, Jamal Musiala dakika ya 47,  Leroy Aziz Sané dakika ya 54 na Erick Choupo-Moting dakika ya 90 na ushei, wakati la wenyeji lilifungwa na Konrad Laimer dakika ya 58.
Bayern Munich inafikisha pointi 10 baada ya ushindi huo na kubaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi mbili na Wolfsburg inayoongoza, wakati  Leipzig inabaki na pointi zake tatu katika nafasi ya 13 baada ya wote kucheza mechi nne.