AUBAMEYANG AING’ARISHA ARSENAL ENGLAND

1 week ago 60

 BAO pekee la mshambuliaji wa kimataifa wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang dakika ya 66 jana limetosha kuipa Arsenal FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Norwich City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa  Emirates Jijini London – huo ukiwa ushindi wa kwanza baada ya The Gunners kupoteza mechi tatu za awali (0-2 Brentford, 0-2 Chelsea, 0-5 Manchester City).